MHARO WA DAMU(Coccidiosis)
Ni ugonjwa unaosambulia zaidi kuku wadogo kutokana hasa kushindwa kusimamia usafi vizuri bandani nakuruhusu maji kumwagika bandani hutokea zaidi wiki ya 2,3,na 4 kwa vifaranga
DALILI
Dalili kuu yeyote ya kuku anaumwa inaonena kwenye kinyesi chake kabla ujachunguza vitu vingine na kwa kuku mwenye ugonjwa huu kinyesi chake huwa cha kahawia au kijivu siku za awali na kisha huchanganyika na damu siku zinavyoenda. zifuatazo ni dalili za kuku mgonjwa
1.kuzubaa
2.kushusha mabawa
3.kupoteza hamu ya kula
4.huharisha chenye rangi ya kahawia mwanzo
5.baadae huharisha choo chenye damu
6.manyoya hutimuka
7.kupauka kwa upanga na ndevu
8.kudhoofika
KINGA
1. kepuka unyevu ndani ya banda
2.kutenga kuku wagonjwa
3.kukinga kwa kutumia cooccidiostat
TIBA
1.Hugonjwa huu utibika endapo hatua za kuthibiti zikichukuliwa mapema
DAWA
1.Amprolium
2.VITA COX
3.AGRA COX
4.ANTCOX
5.Esb3
tumia dawa mojawapo kati ya hizo tajwa pamoja na vitamini kwa ushauri wa mtaalamu
Post a Comment